Tuesday, August 2, 2016

KILIMO CHA NYANYA

mentor tanzania | 9:08 AM



"Nchi yetu ustawi wetu"
Mkulima kumfunza mkulima ,
Ikiwa ni mwndelezo wa Kilimo bora cha nyanya, hapa sasa tayari nyanya imeweka matunda hivyo huhitaji matunzo na maji ya kutosha na kwa wakati pia mkulima hushauliwa kupiga dawa za kuzuia maua yasipukutike , dawa hizo hupatikana kwenye maduka ya pembejeo,
Nyanya huitaji kufungwa vyema waweza ona nyanya ilivyo na matunda ya kutosha nyanya hizi ni F1, ambazo zinalimwa open field tofauti na zile za kwenye vyumba kitaru yaani (green house, screen house) nyanya hizi hatutoi vikonyo maana ukitoa vikonyo upunguza idadi ya matunda cha msingi ni kuweka Mbolea ya kutosha na maji kwa wakati ili mmea upate chakula cha kutosha.
Hapo tunaendelea na zoezi la ufungaji wa kamba ili nyanya isizidiwe matunda na kuanguka kazi hii ni kazi ya kila siku unaangalia nyanya yenye vikonyo vingi na kuongeza fito na kuzifunga pamoja.
Endelea kufatilia Kilimo hichi hakika utajifunza.
 
Share it →

No comments:

Post a Comment

Mentor Tanzania © 2014 |

| Designed By ivan 0759804049