Tuesday, July 12, 2016

KILMO CHA HOHO KINAMKOMBOA MKULIMA.

mentor tanzania | 9:16 AM
KILIMO CHA PILIPILI HOHO
Kilimo cha pipipili Hoho ni kama Kilimo cha mazao mengine ya bustani kama nyanya, tikiti, etc
Katika Kilimo hichi kuna mambo kadha wakadha ya kuzingatia
1. KITARU
Unatakiwa kuandaa kitaru kwa umakini, unahakikisha umelainisha udongo, ili uwe tifutifu, kabla hujapanda unashauriwa kupiga dawa ya fungicide ili kuzibiti magonjwa kwenye udongo KITARU ni sehemu ya kuzingatia sana, katika upandaji wa mbegu zozote, za bustani na ni vyema kutandaza nyasi juu ya KITARU ili kuwepo na unyevu wakotosha ili kulahisisha mbegu kuota vizuri, mbegu za Hoho kutumia siku 8-10 kuota hivyo ni vyema kuzingatia kuweka nyasi na kumwagilia maji ya kutosha
2.MBEGU ZA HOHO
Katika Kilimo cha Hoho kuna kampuni mbali mbali huuza mbegu za Hoho lakini mbegu hizi pia hutofautia kuhimili magonjwa na kuwa na mavuno mengi , vile vile katika zao hili kuna mbegu zinakuwa na marunda makubwa na mengine ya wastani , hivyo ununuzi wa mbegu hizi utegemee aina ya wateja ulionao au SOKO unalotegemea kuuza
Aina nzuri ni yolowander B, na improved variety ambazo husmbazwa na kampuni ya Mkulima,
3.MAGONJWA NA DAWA ZAKE
zao la Hoho husumbuliwa na magonjwa kadhaa lakini ni vyema kuzia magonjwa kuliko kutibu magonjwa yanayosumbua ni ukungu ambapo ni vyema kupiga dawa ya ukungu, kila baada ya wiki moja , dawa hii iendelee kupigwa tangu kwenye kitaru hadi kipindi cha kuanza kuvuna dawa za ukungu ni kama vile ivory 72, linkomil 72, ambayo huzuia na kutibu iwapo zao litakuwa limepata ugonjwa tayari
Madawa mengine ya kuzuia magonjwa mengine ni kama bamic, abamectrin, banophose, Konto, farm guard, etc
KUANDAA SHAMBA ILI KUAMISHA MBEGU (TRANSPLANTING)
Ni vyema kipindi tu unapoweka kitaru uanze uandaaji wa shamba lako ili uweze kuliandaa kwa ufanisi
Katika uandaji huo itakuwemo kuandaa kwa kulima, kupiga halo, na kutengeneza matuta kabla hujapanda unashauriwa kumwagia maji Ardhi ili ipoe kama ni sehemu ya joto Kali sana ikiwemo kuchimba mashimo na kuyawekea Mbolea, zao la Hoho pia huitaji maji ya kutosha kuanzia kupanda hadi kuvuna, Mbolea iweke kulingana na ushauri wa mtalaam alie karibu na wewe,
Naendelea kuelezea zao hili kipindi kingine pia naomba kama kuna watalaam wa Kilimo na wakulima wenzangu tubadilishane utalaam na ushauri ili ndugu na jamaa waweza kunufaika .

Picha ya upandaji wa Hoho na shamba liloandaliwa vizuri
Share it →

No comments:

Post a Comment

Mentor Tanzania © 2014 |

| Designed By ivan 0759804049