Tuesday, July 19, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO YA NYUMBANI

mentor tanzania | 3:43 AM

JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO YA NYUMBANI
Kuna njia mbali mbali waweza kuepuka kutumia mboga mboga zinazolimwa usikokujua na kuepuka kujiingiza katika afya mbaya kwa matumizi ya kemikali za kuulia wadudu na magonjwa zinazotumika katika ukuzaji wa mboga mboga.
Aina za bustani
1. Unaweza tumia makopo amabayo mara nyingi hutumika kupanda maua kando kando ya nyumba
2. Unaweza tumia gunia la sandarusi kubwa..
3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la Ufunguo)
Bustani Ya Makopo/Ndoo
Vifaa
Udongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri.
Udongo – Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk – Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa.
Mbolea ya samadi – Kutoa virutubisho kwa mmea
Hatua za utengenezaji.
– Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk
– Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.
– Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
– Kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo endapo makopo hayo yapo kwene simenti, weka makopo/ndoo hayo juu sahani/besen
Uangalizi.
– Mwagilia mboga yako mara tu baada ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
– Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
– Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
– unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Faida
– Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
– Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
SEHEMU YA PILI YA UTENGENEZAI WA BUSTANI NDOGO ZA NYUMBANI
BUSTANI YA GUNIA
Vifaa
Udongo, Kokoto (mawe madogo madogo), Gunia, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri, mti/mbao na kopo dogo (sadolini).
Udongo – Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk – Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa.
Kokoto – Kusadia maji kupita ndani ya gunia toka juu hadi chini
Mbolea ya samadi – Kutoa virutubisho kwa mmea
mti/Mbao – Kusaidia gunia lako kusimama vyema/ imara
Hatua za utengenezaji.
(i) Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk.
(ii) Toboa kopo lako na ondoa kitako ili kuweka uwazi pande zote mbili (juu na chini)
(iii) Weka mti/ubao katikati ya gunia ukiuchimbia ardhini kisha weka kopo lako katikati ya mti/mbao hiyo na lijaze kokoto
(iv) Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye gunia lako ukilizunguka kopo lenye kokoto hadi kufikia kimo cha kopo. Baada ya hapo ondoa kopo na hakikisha kokoto zinabaki zikizungukwa na udongo.
(v) Weka kopo juu ya kokoto zilizozungukwa na udongo kisha, lijaze kopo hilo na kokoto, rudia kujaza udongo ukilizunguka kopo hadi kimo cha kopo hilo. Endelea kufanya hivyo (kama hapo juu) hadi pale gunia lako litakapokuwa limejaa.
(vi) Toboa gunia kwa kuweka matundu kuzunguka gunia kwa ajili ya kupandia katika umbali sawa (inategemea na aina ya mboga)
(vii) Hapo utakuwa tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote juu na pembeni ya gunia lako
Mboga aina ya letuce (Lactuca sativa)
Mboga aina ya sukumawiki (Brassica carinata) zikiwa zimepandwa kwenye gunia
Uangalizi.
– Mwagilia mboga yako mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
– Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
– Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
– unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Muhimu: Ukitumia miche kwa siku tatu/mbili za mwanzo usije ogopa kuona miche yako imelala endelea kuimwagilia itasimama tu. Pia katika umwagiliaji hakikisha unamwaga maji katika kati ya guni pale kulipo na kokoto ili kuhakikisha maji yanasamba ndani ya gunia hadi chini.
Faidi
– Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
– Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
– inatumia nafasi ndogo na kutoa kiasi kikubwa cha mboga mboga.

TEKNOLOJIA YA UMWAGILIAJI KWA NJIA YA MATONE ITAKUZA KILIMO CHA MATUNDA NA MBOGA KWA WAKULIMA

Mtaalamu wa Mradi wa Kilimo chenye tija Tanzania (TAPP ), Mussa Madurufu ( anayenyosha mikono) akitoa elimu ya namna ya kuendesha wa kilimo cha bustani ya nyanya kwa njia ya teknolojia mpya ya umwagiliaji kwa njjia ya matone wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima Julai 20, 2015 katika bustani ya vipando vya mboga na matunda ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), maonesho yaliyodhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture Tanzania (TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI), na SUA.Ulaji wa matunda ni muhimu kwa afya ya mwili wa binadamu.Baadhi ya Wakulima waliokuwa wakihudhuria maonesho ya wakulima na teknolojia mpya ya umwagiliaji kwa njjia ya matone wakipita kuangalia kipando cha bamia , maonesho hayo yalifanyika julai 20, 2015 , SUA na yalidhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture Tanzania (TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI), na SUA.

Ongeza Kipato chako kwa kufuga kuku


LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
– paraza kilo 25 = 700×25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700×15=10500
– layer’s consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga
Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2×2 au 4×2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Share it →

No comments:

Post a Comment

Mentor Tanzania © 2014 |

| Designed By ivan 0759804049